NUNGU KWA VARWA

 

 

Na Dr Catherine Baroin

 

Wameru (Varwa), ambao ni jamii ya wakulima wenye asili ya Kibantu na waishio katika maeneo ya Mlima Meru (Kaskazini mwa Tanzania), ni watu wenye kuamini na kuhofia sana nguvu ya laana licha ya juhudi za makanisa katika kukemea imani hiyo. Hofu hiyo inatokana na kuamini matambiko ambayo hutumika kama njia ya kupata suluhu ya migogoro baina ya wana jamii baada ya sheria rasmi za nchi kushindwa kupata ufumbuzi. Tambiko hilo linalojulikana kama ‘Kuvunja chungu’ ni kwa ajili ya kuacha laana kwa mtu aliyetenda kosa. Kwa hofu ya kupata laana, mara nyingi mkosaji hukiri makosa na kulipa fidia ya makosa aliyosababisha na kisha hufanyika tambiko jingine kwa ajili ya kupoza laana ya tambiko la awali ili isimuathiri mkosajji ambaye tayari amekwishakiri kosa. Kitini hiki kinalenga kueleza sababu na mazingira yaliyosababisha kuanzishwa kwa utaratibu huu, namna unavyotekelezwa na kisha kitajadili sababu za ufanisi wa utaratibu huo.

Nungu kwa Varwa
2013 Nungu for printer.pdf
Document Adobe Acrobat 219.0 KB